Friday, April 22, 2016

MEYA WA KINONDONI AMFAGILIA DC WA KINONDONI KWENYE KIKAO

MEYA WA KINONDONI AMFAGILIA DC HAPI KIKAONI
Meya wa manispaa ya Kinondoni Mh. Boniphace leo amemuelezea Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuwa ni mtu mwenye historia ya uchapakazi, msimamo usioyumba na mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia uadilifu. Meya ameyasema hayo akifungua kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Kinondoni ambapo alimualika Mh. Mkuu wa Wilaya Ally Salum Hapi kusalimia na kutoa salamu zake kwa baraza hilo. Mheshimiwa Meya Boniphace ameliambia baraza hilo kuwa anamfahamu Mh. Hapi kwakua amesoma nae chuo Kikuu cha Dar es salaam alipokua anasoma masomo ya ualimu.
"Nilimfahamu pale Chuo Kikuu alipokua anasomea Sheria nami ualimu, japo yeye alikua reli ya Kati (CCM) nami nilikua reli ya Tazara (Chadema) tangu wakati huo hadi sasa. Ninamuamini katika uwezo wake na kasi ya uchapakazi. Hakika Rais Magufuli hajakosea kukuteua."

Katika hatua nyingine Meya amemuahidi Mkuu wa Wilaya Hapi ushirikiano wote katika kupambana na changamoto za wananchi wa Kinondoni za madawati, watumishi hewa, ardhi na ufisadi.
Katika salamu zake baada ya kukaribishwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Hapi alimshukuru Mstahiki Meya kwa heshima kubwa aliyompa na kumuahidi kuwa ataiongoza vema Kinondoni katika kutatua kero za wananchi. Hapi alieleza kuwa vipaumbele alivyovitoa Mh. Rais vya watumishi hewa, madawati, afya , usafi na vita dhidi ya rushwa ndiyo mambo ambayo tayari ameanza nayo.
"Siamini kama Kinondoni inaweza kuwa na watumishi hewa 34 pekee. Nimeagiza kazi zaidi ifanyike, na kikao idara ya manispaa ifungue mafaili mapya la uhakiki yenye picha ya kila mtumishi, barua yake ya ajira na nyaraka zote zinazoonesha majukumu yake na aliko. Hii ni katika kubaini nani ni nani, yuko wapi na anafanya nini wakati wa ukaguzi wa ana kwa ana."
Mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni amesema tayari watumishi hewa wasiopungua 10 wamekamatwa na wengine 7 wamelipa fedha kiasi cha milioni 40 walizotia hasara serikali.
"Mchana wa leo nimetaka taarifa ya maandishi kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi juu ya watumishi hewa. Ndani ya saa 1 nikapewa taarifa kuwa tayari hiyo na kuagiza vyombo vya dola viwakamate watumishi hewa waliobakia."
Kuhusu msimamo wake juu ya Kinondoni Mkuu wa Wilaya alisema kuwa Rais amemuamini na kumtuma kuwatumikia wana Kinondoni, na kwamba atafanya kazi hiyo usiku na mchana.
"Nimetangaza vita dhidi ya rushwa, maana Kinondoni inanuka rushwa. Watumishi wote wasio waadilifu wanaoiba pesa za umma na kujinufaisha wao na familia zao nitashughulika nao.
Aidha watumishi wanaomiliki makampuni na kujipa tenda kwa mlango wa nyuma wajiandae, maana nitawasaka popote walipo na sheria itachukua mkondo wake. Hapi alisema sheria na taratibu za utumishi wa umma haziruhusu mtumishi wa umma anayetoa huduma kutangaza tenda ofisini kwake na kisha kuipa kampuni yake au ya familia take.
Akitoa shukrani kwa niaba ya baraza, Mbunge wa Ubungo Saidi Kubenea amemshukuru Mh Mkuu wa Wilaya na kuahidi kumuunga mkono katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
Hata hivyo Mh. Kubenea ametaka sheria na taratibu kufuatwa ili kuhakikisha hakuna mtu anayeonewa katika mapambano hayo.
Baraza la madiwani la Manispaa ya Kinondoni lilikutana leo saa 11 jioni katika ukumbi wa manispaa.

SIFA ZA MWANAMKE WA KUOA

KWA WANAWAKE...!

ARE  YOU WIFE MATERIAL ? (una sifa za kuwa mke?). SOMA HAPA..!!

Ni kwa muda mrefu umelia kutokana na kuumizwa na wanaume, umekuwa na majeraha mengi na vidonda visivyo tibika hadi umefikia hatua ya kuona mapenzi machungu na kutamani kuishi peke yako, pengine umefikia mahali unaona bora utafute mtu wa kuzaa nae tu ila si kuolewa.

'wanaume ni waongo ',' wanaume wote ni wale wale '., mapenzi ya siku hizi hayana maana' 'bora niishi peke yangu ' Ni kauli ambazo mara nyingi unajiambia.. Lakin labda nikuulize ulishawahi kujiuliza kwanin hayo yote yanakupata? Ulishawah kujiuliza tatizo lipo wapi? Kujua tatizo ni nusu ya kupata suluhisho la tatizo.!

Nikusaidie sehemu ambayo wasichana wengi mnafeli, unajua jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia, jinsi unavyo vaa, mambo unayo yawaza na jinsi unavyoongea utavuta aina ya marafiki na wanaume wanaofanana na wewe 'Equal attracts equal' psychology inasema hivyo, au kwa lugha nyingine watalaam wanaita 'law of attraction'.!

Eneo la kwanza la kuangalia, ni jinsi unavyo vaa..! Nguo unazo vaa zinakutambulishaje kwa watu? Nguo za kuacha maziwa yako yote nje, nguo zinakubana na kukuonesha maumbile yako yote mpaka nguo ya ndani uliyo vaa inaonekana, mapaja asilimia kubwa yapo nje.. Kwa uvaaji huu unategemea kupata mwanaume 'decent' wa kukuoa? Je unastahili kupelekwa ukweni na kutambulishwa kuwa ni mchumba na mke wa mtu mtarajiwa? Sikiliza ni kweli uvaaji huo utakufanya kuwavutia wanaume wengi lakini si wa kukuoa, hao wataishia kukusifia mzuri, kukutongoza, kulala na wewe kisha kukuacha.

Hakuna mwanaume anayependa mwanamke wa future anayevaa nguo zisizo na heshima, hata kama atakuambia anakupenda basi atakufanya uwe demu wa kupotezea muda tu na muda wa kuoa ukifika ataku'damp na kumchukua mwingine. Kumbuka 'hata mwizi hapendi kuibiwa'.

Acha kuishi maisha ya tamthilia, acha kujifafanya unaenda na wakati, wakati huwezi kushindana nao utaishia kujishushia heshima yako bure. Mavazi ni kitambulisho kikubwa sana, ukimuona askar utamfahamu kwa kuangalia nguo zake, ukimuona daktari utamfahamu kwa kuangalia nguo zake, mchungaji, shekhe, n. k Je nguo zako zinakutambulisha wewe nani? Kuwa mpole, acha wakati upite wewe baki na heshima yako.!

Jambo lingine la kuangalia ni jinsi unavyo waza na maongezi unayoongea.! Una miaka 2 au 3 upo kwenye uhusiano kila siku maongezi yako ni 'baby umeamkaje', 'umekula? ',' hubby nimekumic ',' leo utanitoa out? ',' kuna blauzi nzuri nimeiona utaninunulia? 'hivi hakuna maongez mengine ya maana ya kuongea mbali na hayo? Kama una umri chini ya 20 una haki kufanya hayo, lakini kama upo zaidi ya hapo dada yangu nakupa Pole. Kama kijana uliye nae wewe ni msichana wake wa 3 au 4 ni kitu gani atakiona kwako cha utofaut ili umshawishi kukuoa akilinganisha na wale wasichana wake waliopita? Be creative dada! Ndoa si kitu Cha mchezo.

Kwanin usitake kujua ana mipango gani kwenye maisha? Kwanin usimshauri kununua kiwanja au kufungua biashara? Kwanin usimuambie mjaribu kupunguza out zisizo na lazima na muweke pesa bank? Utaniambia mambo hayo utayafanya kwenye ndoa ukiolewa, Nyota njema uonekana asubuhi kama sijayaona hayo sasa ya nini kufikiria kuwa na wewe? Jenga ushawishi mapema.!

Unatumia muda mwingi kubadilisha mitindo ya nguo na nywele, kila wigi unataka kununua. Hivi unafikir ukiwa kwenye ndoa tutakula wigi lako? Na hayo makucha uliyofuga utaweza kunifulia nguo kweli? Utaweza kufua nepi za watoto? Si utaniambia nitafute msichana wa Kazi au washing machine mikono itachubuka? Sikiliza dada yangu nikuambie hakuna furaha kwa mwanaume kama kumuona mke wake akimfulia nguo, kunyosha nguo zake, kumpikia n. k hata kama si kila siku lakini atapenda akuone ukifmfanyia  hayo pindi ukipata nafasi na si binti wa Kazi.

Unataka kuolewa na mwanaume mwenye pesa ili upate mtelemko, Sikiliza dada hakuna mwanaume anayependa goalkeeper hata kama ana uwezo, nowdays wanaume wanataka wanawake ma'fighter kwa lugha ya kisaa wanasema 'jembe'. Badilika, jirembe sawa lakini usisahau kuuremba uzuri wako wa ndani ambao ni UFAHAMU wako kama mwanamke.! Uzuri wako bila kuwa na akili nzuri biblia inafananisha na kitu Cha THAMANI kilicho sehemu ya OVYO isiyo na HESHIMA.

"mwanamke mzuri asiye na akili ni kama Pete ya DHAHABU puani mwa NGURUWE " Mithali 11:22..!

Hapa sijaongolea kuhusu lugha za mkato unazo mjibu mpenzi wako, kiburi, hasira na kununa bila sababu za msingi, kuruhusu mwanaume kulala na wewe kabla ya ndoa (NA HAPA KUNA SHIDA SI KIDOGO) muda haunitoshi kuyaongolea hayo kwa sasa, Mungu akipenda tutayaangalia siku nyingine. lakin kwanin mwanamke? Kwa sababu wewe ndio muhimili mkubwa wa ndoa, kusimama au kuvunjika kwa ndoa kuna kutegemea wewe. Ndoa itapona kwa HEKIMA yako na itavunjwa na UPUMBAVU wako.!

Naomba niishie hapa kwa leo...!

BE STRONG WOMAN, BE WOMAN OF PRINCIPLES, BE A GOOD WIFE, BE A ROLE MODEL TO YOUR CHILDREN.!

kumuelimisha mwanamke ni  kuelimisha jamii, I HOPE NIMEELIMISHA JAMII.!

# WANAWAKE MNAWEZA MKIJITAMBUA #

(share kwa wanawake wengine)

Na Mwl John Charles Ntogwisangu.

Thursday, April 21, 2016

Deput Minister HAMISI KIGWANGALLA Akikagua Hospital Kilimanjaro

Akikagua theatre ya hosipital ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi Hospital.Hii nimoja ya theatre ya kisasa kabisa nchini sambamba na mradi huu aalikagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya ya hospitali ya Mama na matoto

ZIARA YA VIONGOZI WA SHIRIKISHO ELIMU YA JUU DODOMA

Shirikisho la elimu ya juu lililo anzishwa may 14 -2012 kwa malengo ya kusimamia haki na matatizo ya wanafunzi wa elimu ya juu kama vile mikopo na ajira

Mwenyekiti shirikisho elimu ya juu Tanzania akiwa kwe ziara katika tawi la hombolo mkoani DODOMA


Viongozi wa tawi la hombolo wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa shilikisho la elimu ya juu Tanzania Bi ZAINABU ABDALLAH pia 

FAREED MUSA wa Azam kuelekea Hispania leo kwa Majaribio

winga chipukizi wa klabu ya Azam fc Fareed Mussa (wa katikati) leo hii anatarajia kuondoka nchini hapa na kuelekea Hispania kwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa
    Fareed huko atafanya majaribio na timu za MALAGA na LAS PALMAS Atarejea tanzania may 19

Real Madrid to offer Cristiano Ronaldo new £16.5m-a-year contract after U-turn on star forward's future

Real Madrid look set to complete their U-turn on the future of Cristiano Ronaldo by offering him a contract extension that will keep him at the club until he is 35. 
Madrid president Florentino Perez started the season with the intention of cashing in on Real's all-time record goalscorer with Paris Saint-Germain ready to pay close to €100million (£80m) for his services.
But Ronaldo has broken the 30-goal barrier for the sixth straight season and Gareth Bale - the man Perez wants to replace the Portuguese star as Madrid's talisman - has again missed part of the season through injury.
There is unlikely to be any great change to Ronaldo's current £16.5m per year salary, rather Madrid have prioritised simply extending his stay at the club. 
Real Madrid look set to offer star striker Cristiano Ronaldo a new contract to keep him at the club until 2020
Real Madrid look set to offer star striker Cristiano Ronaldo a new contract to keep him at the club until 2020
The Portugal captain has been in prolific form this season and the Spanish giants are keen to retain him
Madrid need to buy big this summer because a FIFA transfer ban will begin in January 2017 and they need to raise money to fund the spending. 
Flogging Ronaldo whose current deal runs out in 2018 looked like being the best way of doing that. 
But there has been a change of plan at the Santiago Bernabeu and Colombian midfielder James Rodriguez and Spanish forward Isco now look like being the highly-priced sacrifices.

Mkuu wa wilaya ya kinondoni ALLY SALUM Akiapishwa

Mkuu wawilya mpya Bwana ALLY SALUM ameapishwa Leo katika ofisi za  mkuu wa mkoa wa Dar es saal

        SwaggssTV news room